Jumanne March 18 katik uwanja wa KMC Complex, mchezo wa duru ya pili ligi kuu ya Wanawake kati ya Simba Queens dhidi ya Yanga Princess utapigwa uwanja wa KMC Complex
Baada ya kaka zao kukimbia March 08 pale uwanja wa Benjamin Mkapa, bila shaka dada zao hawatakuwa na kipengele, watapeleka timu KMC Complex
Yanga Princess inakwenda katika mchezo huu ikiwa na kiwango bora pengine kuliko wakati mwingine wowote katika misimu mitatu iliyopita
Maboresho makubwa yalifanyika katika usajili w dirisha dogo na sasa matunda yake yameanza kuonekana
Yanga Princess ilianza msimu kwa kusuasua lakini sasa imepania kumaliza mechi zilizosalia kibabe
Kinadada hao Wananchi wametoka kutwaa taji la Samia Super Cup mkoani Arusha wakiichapa JKT Queens mabao 3-0 katika mchezo wa fainali
JKT Queens iliiondosha Simba Queens kwa kuichapa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali huku Yanga Princess ikiifumua Fountain Gate Princess mabao 7-0 katika mchezo wa nusu fainali
Simba Queens walimaliza wa tatu katika michuano hiyo wakiifunga Fountain Gate Princess mabao 2-1 katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu
Ni wazi mechi ya kesho Yanga Princess watacheza wakiwa na dhamira moja tu, USHINDI
