Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema mechi ya kirafiki dhidi ya Singida Black Stars imekuja wakati mwafaka ambapo anaamini mchezo huo utairejesha timu yake kwenye ari ya ushindani baada ya mapumziko ya wiki moja
Yanga ilirejea mazoezini juzi kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa Jumatatu katika uzinduzi wa uwanja wa Singida Black Stars huko Singida
Hamdi amesema ni wakati sahihi wa wachezaji wake kuonyesha uwezo hasa wale ambao wamekuwa wakikosa nafasi ya kucheza.
"Natarajia mchezo mzuri na bora kutoka kwa Singida Black Stars kutokana na kuwa na nyota wengi bora na wazoefu, naifahamu vizuri timu hiyo pamoja na kwamba sipo hapa nchini muda mrefu"
"Ni kipimo kizuri kwetu na ni muda sahihi kupimana nao nguvu na kubaini ubora wao na mapungufu yao yakiwa ni maandalizi sahihi ya michezo yetu ijayo ya ligi," alisema Hamdi
Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kesho Jumamosi kuelekea Singida kwa kupitia mkoani Dodoma
Baada ya mchezo huo Wananchi watarudi Dar kujiandaa na mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Songea United utakaopigwa March 29 uwanja wa KMC Complex