Wanachama Geita waunga mkono msimamo Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Mar 2025
Wanachama Geita waunga mkono msimamo Yanga

Umoja wa Matawi 12 ya wanachama wa Klabu ya Yanga mkoani Geita wameunga mkono uamuzi wa viongozi wao kutocheza mchezo mwingine wa dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Maazimio ya wanachama hao yalitolewa juzi mbele ya waandishi wa habari baada ya kuitisha mkutano wa dharura mjini Geita na kusisitiza kwa kauli moja kuwa wanataka kuona haki inatendeka

Mratibu wa Matawi ya Yanga Mkoa wa Geita, Rajab Mohamed akisoma maazimio ya wanachama wa Yanga Geita amesema uamuzi uliotolewa na Rais na Makamu wa Rais wa Yanga ni sahihi

"Wanachama na mashabiki wa Yanga ndani ya mkoa wa Geita, tunaungana na viongozi wetu wa makao makuu, hatuhitaji busara kutatua mgogoro huu unaoendelea"

"Tunaamini bodi ya ligi inaongozwa na sheria pamoja na kanuni zake, basi viongozi wa bodi ya ligi kutatua huu mzozo na siyo watuambie masuala ya busara na hekima"

"Kama Yanga amevunja sheria ama Simba amevunja sheria, basi TFF na bodi ya ligi wakae chini wapite hizo sheria," alisema Rajabu

Ameongeza, pia wanachama wa Yanga mkoani Geita hawana imani tena na uongozi wa bodi ya ligi na wanamtaka Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuacha kutoa kauli za kebehi na uchochezi

Wanachama wa Yanga kutoka mikoa mbalimbali wanaendelea kutoa matamko kuunga mkono msimamo wa viongozi wao kufuatia bodi ya ligi kuahirisha mchezo dhidi ya Simba uliopaswa kupigwa March 08 pasipo sababu za msingi

Mikoa ya Kigoma, Dar es salaam, Zanzibar na Pwani Wanachama wake wametoa matamko ya aina hiyo huu ukiwa msimamo wa mashabiki na wanachama wa Yanga nchi nzima

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’