Jumamosi March 29 katika uwanja wa KMC Complex, Yanga itakuwa mwenyeji wa Songea United katika mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la CRDB
Ni mechi nyingine ambayo matokeo ya ushindi yatawahakikishia Wananchi kutinga robo fainali ya michuano hiyo ambayo Yanga inacheza ikiwa mabingwa watetezi
Yanga imeweka rekodi ya kushinda mechi 20 mfululizo katika michuano hiyo, ushindi dhidi ya Songea United utaongeza utamu wa rekodi hiyo
Msimu huu Yanga inalisaka taji la nne mfululizo huku ikiwa na rekodi ya kucheza fainali nne mfululizo za michuano hiyo
Kikosi cha kocha Miloud Hamdi kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo huo huku msemaji wa Yanga Ali Kamwe akitamba watashusha full-squad kuikabili Songea United

ADVERTISE HERE