Kikosi cha Yanga kimerejea mchana wa leo Jumanne kutoka nchini Algeria ambapo kilicheza mchezo wa kwanza wa kundi D kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger na kupoteza kwa mabao 4-0.
Baada ya kuwasili Yanga inatarajiwa kusafiri kwenda mkoani Mbeya kesho kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Prisons, May 10.
Siku tatu baadae, May 13 Yanga itakuwa mkoani Morogoro kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya vodacom.
Baada ya michezo hiyo miwili, Yanga itarejea jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo wa pili wa kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports May 16.

ADVERTISE HERE