Jumamosi March 29 kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili Songea United katika mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la Shirikisho la CRDB
Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amefichua katika mchezo huo hatawatumia nyota waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa
Hamdi ambaye siku ya Jumatatu kikosi chake kilikuwa mkoani Singida katika uzinduzi wa uwanja wa Airtel wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya wamiliki wa uwanja huo Singida Black Stars, alieleza kufurahishwa na kiwango kilichooonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo huo
Kwani licha ya kuwakosa wachezaji 10, waliwapa upinzani Singida Black Stars katika mchezo ambao haukumalizika baada ya mvua kubwa kunyesh iliyoambatana na upepo mkali
Hamdi amesema kama wachezaji watajituma na kufuata vyema maelekezo, watashinda mchezo dhidi ya Songea United
"Tulikwenda Singida bila wachezaji 10 tegemeo, hivyo kwetu ilikuwa ngumu sana, lakini walicheza vyema dhidi ya timu yenye wachezaji bora iliyokamilika ya Singida Black Stars, kwa maana hiyo hawa wachezaji kama nikiwachezesha dhidi ya Songea United wanaweza kunipa ninachokihitaji"
"Tunakabiliwa na uchovu, nadhani hata wachezaji watakaotoka kwenye vikosi vya timu za taifa pia watakabiliwa na uchovu, kwa maana hiyo katika mchezo huo nitatengeneza mazingira ya 'kubalansi' kuchezesha nyota ambao wamepumzika na dakika chache wale ambao wametoka kwenye mechi za kimataifa na kusafiri kwa umbali mrefu," alisemaHamdi
Aliongeza kwa sasa ameshakiandaa kikosi chake kwa ajili ya kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya mashindano hayo ya FA
Yanga ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo ikibeba taji hiloo Juni 2, mwaka jana kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, baada ya kuifunga Azam FC penalti 6-5 kufuatia matokei ya suluhu waliyopata ndani ya dakika 120
Baada ya mchezo dhidi ya Songea United, Yanga itasafiri mkoani Tabora kuikabili Tabora United katika mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaopigwa April 1 katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi