Zahera ashauri Yanga B ikacheze na Prisons, Mtibwa Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
9 May 2018
Zahera ashauri Yanga B ikacheze na Prisons, Mtibwa Sugar
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ameshauri uongozi kupeleka kikosi cha timu ya vijana, maarufu kama Yanga B katika mechi zake mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons mjini Mbeya na Mtibwa Sugar mjini Morogoro, ili kikosi cha kwanza kiendelee na maandalizi ya mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Jumatano ijayo.

Zahera amesema kwa sasa Yanga wanapaswa kuelekeza nguvu zao kwenye mechi za Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya kupoteza nafasi ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu.

Zahera ameyasema hayo leo mchana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam wakati kikosi cha Yanga kikiwasili kutoka Algiers nchini Angeria ambako Jumapili kilifungwa mabao 4-0 na wenyeji, U.S.M. Alger katika mchezo wake wa kwanza wa Kundi D Kombe la Shirikisho Uwanja wa Julai 5, 1962.

“Hatuna nafasi kwenye ligi, hivyo tunatakiwa kuweka nguvu zote kwenye kombe la Shirikisho, nimewaomba viongozi wapeleke kikosi B katika michezo yetu ya ligi, ili nibaki na kikosi cha kwanzaa nikiandae kwa ajii ya mchezo dhidi ya Rayon”.

"Tunatakiwa kujiandaa vema ili tusipoteze mchezo huo, ukiangalia ratiba ya ligi imekaa vibaya kwetu, tumefika leo, kesho tunatakiwa kwenda Mbeya, baadaye tuna mchezo Morogoro, kabla ya kuivaa Rayon, ndio maana nimewaomba wakubwa tuwaze zaidi kombe la Shirikisho,”amesema.

Akizungumzia kipigo cha Algeria, Zahera alisema kikosi chake kiipoteza mchezo huo kutokana na kukosa wachezaji wazoefu.

“Tulipoteza mchezo kwa kukosa uzoefu, hatukuwa na wachezaji wetu wazoefu, hivyo uwanjani tulikuwa na watoto watano, wenzetu walitumia mwanya huo kutuadhibu.

"Kwenye mpira uzoefu ni jambo la msingi, vijana walijitahidi kucheza kwenye majukumu waliyopewa, lakini walikosa umakini,”alisema.

Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →