Mahakama ya Kimataifa ya usuluhisho ya Michezo (CAS) imetoa siku 10 kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi (TPLB) na klabu ya Simba kuandaa na kuwasilisha utetezi wao kabla ya Mahakama hiyo kuanza kusikiliza kesi dhidi yao
Yanga ilifungua kesi CAS kupinga kuahirishwa kwa mchezo namba 184 ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopaswa kupigwa March 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Katika kesi hiyo Yanga inatarajiwa kuwakilishwa na Mawakili watano ambao ni;
- Alex Mgongolwa
- Simon Patrick
- Juma Nassoro
- Respicius Didace
- Kalaghe Rashid



ADVERTISE HERE