Wananchi wanahesabu masaa kabla ya kushuka uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora kuwakabili wenyeji wao Tabora United katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa lengo moja tu, kuchukua alama zote tatu mbele ya Tabora United ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo
Habari njema ni kuwa Yanga inakwenda katika mchezo huo huku safu yake ya ushambuliaji ikitarajiwa kuongozwa na vinara wake wa kuzifumania nyavu Prince Dube na Clement Mzize
Mzize na Dube kila mmoja amepachika mabao 10 na pengine leo watakuwa na nafasi ya kuongeza idadi yao ya mabao. Wote wamerejea kutoka kwenye majukumu ya timu za Taifa wakiwa 'fit'
Licha ya kumkosa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki, uwepo wa Maxi Nzengeli na Pacome Zouzoua unaendelea kuwahakikishia Wananchi nafasi za kufunga mabao zitatengenezwa kwa wingi
Maxi ametoa asisti 7 msimu huu kama ilivyo kwa Aziz Ki huku Pacome akiwa na asisti 6 na mabao 7 ya kufunga. Dube licha ya kufunga mabao 10, pia ametoa pasi 7 za mabao
Eneo la kiungo Mudathir Yahya anatarajiwa kurejea na pengine Salum Aboubakar 'Sure Boy' au Duke Abuya mmoja wao atachukua nafasi ya Khalid Aucho ambaye alipata changamoto ya misuli alipokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa
Eneo la safu ya ulinzi pia limeimarika, Ibrahim Bacca na Dickson Job wote wakirejea salama kutoka majukumu ya timu za Taifa
Ikumbukwe katika mchezo wa duru ya kwanza ambao Yanga ilipoteza kwa mabao 3-1, Bacca na Job walikosekana. Bacca alikuwa akitumikia adhabu ya kadi nyekundu huku Job akiuguza majeraha
Ni wazi Yanga leo inakwenda kupambana na Tabora United ikiwa bora zaidi kuliko ilivyokuwa mara ya mwsho timu hizo zilipokutana dimba la Azam Complex Tabora United wakishinda mabao 3-1
Tangu Yanga ipoteze mchezo dhidi ya Tabora United, haikupoteza mchezo mwingine tena wakitoka sare mechi moja tu dhidi ya JKT Tanzania