Baada ya kushikiliwa kwa saa kadhaa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ameachiwa kwa dhamana
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora SACP Richard Abwao amethibitisha kuachiliwa kwa Ofisa huyo wa Klabu ya Yanga mchana wa leo
Kamwe alikamatwa jana majira ya saa saba usiku kwa ajili ya mahojiano, kufuatia kauli alizozitoa kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United
Anatuhumiwa kutoa kauli za kebehi kwa viongozi wa Serikali na Mamlaka za uteuzi Aprili Mosi wakati akizungumza mashabiki na Wanachama wa Yanga katika viwanja vya Chipukizi mjini Tabora
Ametakiwa kuripoti mkoani Tabora April 21 mwaka huu
ADVERTISE HERE