Mechi sita za kuhitimisha msimu NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Apr 2025
Mechi sita za kuhitimisha msimu NBC PL

Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United, mabingwa watetezi ligi kuu ya NBC Yanga wanaendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo

Yanga imesalia na mechi sita tu za kuhakikisha ubingwa unarejea Jangwani kwa mara nyingine. Hapa hatujahesabu mechi dhidi ya Simba ambayo Yanga imeweka wazi msimamo wake wa kutocheza huku ikiwa tayari imefungua kesi CAS dhidi ya waliokwamisha mchezo huo kuchezwa March 08

Jumatatu April 07 Wananchi watashuka dimba la KMC kuikabili Coastal Union na April 10 watakuwa Azam Complex kumenyana na Azam Fc

April 20 Yanga itakuwa Manyara kumenyana na Fountain Gate kabla ya kikosi kuelekea Zanzibar kushiriki ligi ya Muungano

Mechi tatu za kuhitimisha msimu zitapigwa May dhidi ya Namungo (May 13 - KMC Complex), Prisons (May 21 - Sokoine) na Dodoma Jiji (May 25 - KMC Complex)

Katika mechi sita zilizosalia, Yanga itatoka nje ya jiji la Dar es salaam mara mbili kuzikabili Fountain Gate na Tanzania Prisons na mechi nne zilizosalia zitapigwa jijini Dar es salaam

Mkakati wa Yanga ni kutwaa mataji yote matatu ya ndani Wananchi wakiwa tayari wameweka Ngao ya Jamii kabatini

Katika michuano ya kombe la Shirikisho la CRDB Yanga iko hatua ya robo fainali ikisubiri kucheza na Stand United

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’