Pacome anaamini ubingwa ni suala la muda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Apr 2025
Pacome anaamini ubingwa ni suala la muda

Kiwango bora kinachoendelea kuonyeshwa na Yanga huku ikipata ushindi mfululizo ugenini na nyumbani, imempa jeuri kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Yanga, Pacome Zouzoua ambaye amesema kuwa hawaoni timu ya kuwazuia kutetea taji la Ligi Kuu Bara msimu huu

Pacome ambaye amehusika kwenye mabao 16 msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara akifunga saba na kutoa asisti 9, amesema ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Tabora United umedhihirisha kwa sasa hawana utani na malengo yao ya kutetea ubingwa

"Yanga ni ile ile ya msimu uliopita, kitu kikubwa kilichobadilika ni kwa wachezaji pekee ambao kila mmoja anaonyesha kujipambania na kuipambania timu, hivyo ukiunganisha unapata timu bora na ya ushindani"

"Hicho ndicho kinachofanyika sasa na naamini kwenye mechi zilizobaki tukichanga vizuri karata zetu tutaendelea tulipoishia"

"Kila mechi iliyo mbele yetu tunaichukulia kama fainali, tunawaheshimu wapinzani wetu wote, hakuna timu changa wala kongwe kwenye ligi, tunaamini katika ushindani. Malengo yetu kwa sasa ni kukusanya pointi kwenye kila mchezo hivyo imani kubwa ni maandalizi bora bila kujali tunakutana na timu ya aina gani," amesema Pacome

Kiungo fundi huyo ambaye kwa upande wa Yanga anaongoza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo msimu huu akichukua mara tano, alisema wanatambua ubora wa wapinzani walio mbele yao kwenye mechi zilizobaki lakini hawana hofu kutokana na ubora na malengo waliyojipangia kuhakikisha wanatetea taji la ligi

Akizungumzia ubora wake kwa ujumla, raia huyo wa Ivory Coast alisema unachangiwa na morali nzuri ya kikosi cha timu hiyo ambacho ameweka wazi kuwa wanacheza kwa kushirikiana na kuipambania timu ambayo ina malengo makubwa kuhakikisha inakuwa bora ndani na kimataifa

"Ushirikiano mzuri ninaoupata kutoka kwa wenzangu na pia kuaminiwa na benchi la ufundi licha ya ushindani mkubwa wa namba kwenye eneo ninalocheza, ndio kitu kinanifanya nipambane na kumuonyesha kocha kuwa hajakosea kunipa nafasi kwa kufanya majukumu yangu kwa ubora," alisema

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’