Baada ya kukosekana dimbani kwa takribani miezi mitatu akiuguza majeraha, mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi amerejea
Yao ameanza kufanya mazoezi ya timu baada ya kumaliza program maalum ya mazoezi binafsi
Ni wazi sasa kocha Miloud Hamdi anaweza kuanza kumtumia na yawezekana leo katika mchezo dhidi ya Coastal Union akapata dakika chache
Hata hivyo Yao anarejea katika nyakati ambazo Israel Mwenda amejimilikisha eneo la ulinzi upande wa kulia akifanya vizuri
Yanga ilimsajili Mwenda dirisha dogo baada ya kuumia kwa Yao na tangu amesajiliwa, amepenya moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza
Unaweza kusema kazini kwa Yao sasa kuna kazi, kwani mbali na Mwenda, Kibwana Shomari nae yuko fit akisubiri nafasi yake
ADVERTISE HERE