Uongozi wa klabu ya Yanga, umetoa mapumziko ya wiki mbili kwa kikosi cha Yanga Princess baada ya ligi kuu ya Wanawake kusimama kwa takribani mwezi mmoja
Mratibu wa Yanga Princess, Kibwana Matokeo amesema mapumziko hayo yalitolewa tangu wiki iliyopta (March 31), na watarejea kambini Aprili 15 kwa ajili ya mechi za kumaliza msimu
Timu hiyo iko nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 33, ikicheza mechi 15, ushindi mechi 10, sare tatu na kupoteza mbili.
Matokeo amesema baadhi ya wachezaji hawakusheherekea sikukuu na familia zao hiyo pia ni sababu ya kutoa mapumziko hayo
"Wachezaji wako likizo hadi tarehe 15 watakapoanza maandalizi ya kumaliza ligi, kuna umuhimu mkubwa wa kutoa likizo kwa wachezaji kutokana na wanachokifanya uwanjani miili nayo inahitaji mapumziko," alisema Kibwana