Tutapambana kushinda dhidi ya Azam Fc - Miloud

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Apr 2025
Tutapambana kushinda dhidi ya Azam Fc - Miloud

Kocha mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi, amesisitiza umuhimu wa kupata alama tatu muhimu huku kikosi chake kikijiandaa kukutana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaochezwa Alhamisi, Aprili 10, katika Uwanja wa Azam Complex, saa 1 usiku


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo huo, Hamdi alieleza kuwa ushindi dhidi ya Azam FC utasaidia kuimarisha nafasi ya Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi na kuwaweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo.


"Tunahitaji kushinda mchezo huu, na tutafanya kila kitu kuhakikisha tunashinda," alisema Hamdi


Yanga kwa sasa inaongoza Ligi Kuu ya NBC na iko katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao. Hata hivyo, Hamdi alisisitiza kuwa bado kuna kazi kubwa mbele yao na hawapaswi kubweteka.


Kocha huyo pia alitumia fursa hiyo kumzungumzia kwa heshima kocha wa Azam FC, Rachid Taoussi, ambaye amekuwa rafiki yake wa muda mrefu.


"Nimefahamiana na Taoussi kwa zaidi ya miaka 15. Ni kama kaka yangu," alisema Hamdi. "Ni kocha mzuri na namheshimu sana."


Hamdi alikiri kuwa Azam FC ni timu ngumu na itakuwa na hamasa kubwa ya kupata ushindi, hasa ikizingatiwa kuwa inawania nafasi ya tatu ili kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup) msimu ujao.


"Azam watakuwa na kiu ya kushinda mchezo huu. Wanahitaji pointi hizi ili kuendelea na matumaini ya kufuzu CAF, na tunajua watapambana kwa nguvu," aliongeza.


Licha ya ushindani unaotarajiwa, Hamdi alisema kuwa malengo ya Yanga bado yako wazi—kutetea ubingwa wa Ligi Kuu.


"Tunajua presha iliyopo, lakini tumejipanga vizuri. Ushindi katika mchezo huu utatuweka katika nafasi nzuri sana kuelekea mechi za mwisho wa msimu"


Mchezo kati ya Yanga na Azam FC unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki na wadau wa soka nchini, kwa kuwa timu zote mbili zinahitaji ushindi kwa sababu tofauti


Kwa Yanga hii ni kama mechi ya kulipa kisasi baada ya kupoteza mechi ya duru ya kwanza wakifungwa bao 1-0

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’