Aziz Ki kuendeleza rekodi ya mabao dhidi ya Azam Fc?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2025
Aziz Ki kuendeleza rekodi ya mabao dhidi ya Azam Fc?

Habari njema kwa wapenzi na mashabiki wa Yanga ni kwamba leo kuna uwezekano mkubwa wakamshuhudia kiungo mshambuliaji Stephane Aziz katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa uwanja wa Azam Complex

Ni baada ya kukosekana katika mechi mbili mfululizo zilizopita akisumbuliwa na maumivu ya mgongo

Aziz Ki ambaye mara ya mwisho alitokea benchini Machi 29 mwaka huu wakati Yanga ikiifunga Songea United mabao 2-0 kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho (FA) hatua ya 16 bora, alikosekana katika mechi mbili zilizopita za ligi ambazo Yanga ilizifunga Tabora United (3-0) na Coastal Union (1-0).

Nyota huyo wa Kimataifa kutoka Burkina Faso ambaye hivi karibuni amefunga ndoa na mrembo Hamisa Mobeto, amesema kwa sasa ameimarika kwani licha kutoonekana uwanjani alikuwa akifanya mazoezi

"Mechi zilizopita sikufanikiwa kucheza, lakini nilikuwa nafanya mazoezi kama kawaida, hivyo muda wowote mashabiki wategemee kuniona kazini," alisema Aziz Ki ambaye msimu uliopita alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara akifunga mabao 21.

Kiungo huyo ambaye huu ni msimu wake wa tatu kuitumikia Yanga, amekuwa na rekodi nzuri ya kuifunga Azam kwani mara tano alizokutana nayo kwenye ligi amefunga mabao manne ikiwemo hat trick moja.

Kwa ujumla, Aziz Ki amecheza dhidi ya Azam mara tisa kwenye michuano tofauti, akifunga mabao sita ambapo manne kwenye ligi na mawili Ngao ya Jamii, huku akishindwa kufunga katika Kombe la FA. Kwenye ligi, Aziz Ki amecheza dhidi ya Azam mara tano, FA (2) na Ngao ya Jamii (2).

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’