Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Azam Fc
Mchezo huo utakaopigwa saa 1 usiku, alama tatu zinaweza kuiweka Yanga katika nafasi nzuri zaidi katika mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu
Ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi ikikusanya alama 64, ushindi utawahakikishia Wananchi kuongoza ligi kwa tofauti ya alama 10 na kusalia na mechi nne za kutetea ubingwa wao
"Niwaombe mashabiki wa Yanga tujitokeze kwa wingi uwanja wa Azam Complex kuiunga mkono timu yetu"
"Kimsingi hii ni mechi ngumu ambayo kwa kiasi flani inaweza kutupa mwanga wa hatma yetu katika kutetea ubingwa"
"Tuje kwa wingi uwanjani na pia tushangilie sana wachezaji wetu katika muda wote wa mchezo ili kuwaongezea hamasa"
"Huu ni mchezo ambao tunaona unaweza kuwa na maamuzi ya furaha yetu msimu huu hivyo tunakwenda kukabiliana nao kwa nguvu kubwa kama tulivyofanya katika mechi nyingine kubwa tulizocheza"
"Tunakwenda kucheza kikubwa tukiwa na ari kubwa na naamini tutakwenda kupata matokeo mazuri," alisema Kamwe