Baada ya ushindi muhimu dhidi ya Azam Fc na kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 10, kikosi cha Yanga sasa kinaelekeza nguvu zake katika mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Stand United
Jumanne, April 15 katika uwanja wa KMC Complex, Yanga itaikaribisha Stand United katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wanatambua ubora wa Stand United hivyo hawauchukulii mchezo huo kwa wepesi
"Tuna dhamira ya kutetea taji la CRDB kwa msimu mwingine, Jumanne tunakwenda kucheza mchezo wa robo fainali dhidi ya Stand United"
"Tunatambua ubora wa Stand United, hatuwezi kuwadharau kwa kuwa wanatoka ligi ya Championship"
"Kwa wale wanaofuatilia Championship, wanafahamu ugumu wa Stand United hivyo tunafahmu aina ya mechi tunayokwenda kukabiliana nayo," alisema Kamwe
Yanga ndio mabingwa watetezi wa taji la CRDB wakitwaa taji hilo kwa misimu mitatu mfululizo
Aidha Wananchi watakuwa wakisaka nusu fainali ya tano mfululizo