Hamdi 'apagawa' ubora wa Chama

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2025
Hamdi 'apagawa' ubora wa Chama

Baada ya kuonyesha kiwango bora katika michezo miwili iliyopita, Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema hana mashaka na uwezo wa kiungo fundi Clatous Chama, ni mmoja ya wachezaji muhimu katika kikosi chake

Tangu ujio wa Hamdi aliyechukua nafasi ya Sead Ramovic, Chama amepata nafasi finyu ya kuanza katika kikosi cha kwanza

Hata hovyo Hamdi alimuanzisha katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Azam Fc na Stand United na zote akan'gara

Hamdi amesema anafurahi kuona kila mchezaji anapopewa nafasi anaipambania Yanga, Chama amepewa nafasi na amedhihirisha ubora wake

"Chama ni mchezaji mzuri kila mmoja anafahamu, anapokuwa katika ubora wake nafikiri ni mchezaji ambaye sio rahisi kumzuia"

"Amekuwa katika ubora mzuri katika mechi mbili zilizopita, nafikiri ni jambo jema kwa timu nzima mchezajia anapopewa nafasi na kufanya vizuri"

"Sio Chama tu, kuna wachezaji wengine kama Farid Mussa, Kennedy Musonda, Kibwana Shomari nao wamefanya vizuri katika mechi iliyopita," alisema Hamdi

Chama amerejea kikosi cha kwanza na kutumia vyema nafasi hiyo katika nyakati ambazo Yanga inawakosa Khalid Aucho na Pacome Zouzoua wakiwa majeruhi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’