Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana kwa ajili ya kupitia na kutoa uamuzi wa mashauri yaliyowasilishwa mbele yake
Miongoni mwa mashauri hayo ni shauri lililomuhusu Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ambaye alituhumiwa kwa kosa la kuchochea UMMA
Katika maamuzi yake, Kamati imemtia hatiani Kamwe na kumpa adhabu ya kulipa faini ya Tsh Milioni 5 pamoja na onyo la kutofanya kosa la kimaadili ndani ya kipindi cha miaka miwili
Adhabu kama hiyo imewakumba Afisa Habari wa Kagera Sugar Hamis Mazanzala, huku Ahmed Ali wa Simba akikosekana na hatia
ADVERTISE HERE