Kwa Yanga hii watalalamika sana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Apr 2025
Kwa Yanga hii watalalamika sana

Kuna wachambuzi wanatumika kueneza propaganda baada ya ushindi wa mabao 4-0 ambao Yanga waliupata dhidi ya Fountain Gate jana

Wachambuzi hao wanataka ionekane Yanga haikushinda kihalali mchezo dhidi ya Fountain Gate wakitumia makosa yaliyofanywa na mlinda lango John Noble katika mabao mawili ya mwanzo

Ni hivi; ushindi wa Yanga jana ni kama umevuruga matarajio ya timu ile ambayo ilipewa likizo ya kutocheza mechi zao za ligi kuu wakisubiri Wananchi wadondoshe alama

Mechi zote nne Yanga imeshinda zikiwemo mechi dhidi ya Tabora United na Azam Fc ambazo waliweka matumaini Wananchi wanaweza kutereza. Sasa zimebaki mechi tatu, mbili zikiwa nyumbani na mechi moja tu itachezwa ugenini

Chini ya kocha Miloud Hamdi, Yanga imecheza mechi 12 na imeshinda mechi 11 huku ikitoka sare mechi moja tu

Yanga imecheza jumla ya mechi 21 katika mashindano yote bila ya kupoteza! Ivi kuna aliyeamini Fountain Gate ingeweza kuizuia Yanga hii ambayo magoli yanatoka kila upande?

Noble sio mlinda lango wa kwanza kufanya makosa, hata yule wao si alifanya makosa katika ile dabi ya kwanza waliyojifunga? Msimu uliopita Noble akiwa Tabora United nao si walinufaika na makosa yake?

Lakini pia, kama tatizo alikuwa Noble mbona hata alipoingia Parapanda nae akifungwa mabao mawili?

Kwa hakika msimu huu Yanga imepigana vita ya aina yake, na bila shaka ushindi umekaribia..!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
11h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
15h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
16h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
16h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’