Kombe la Muungano kupigwa Pemba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Apr 2025
Kombe la Muungano kupigwa Pemba

Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), limehamisha uwanja wa mashindano ya Kombe la Muungano na sasa yatachezwa katika Uwanja wa Gombani, Pemba.

Awali, shirikisho hilo lilitangaza kuwa mashindano hayo yataanza, Alhamisi, Aprili 24, 2025 katika Uwanja wa New Amaan Complex mjini Unguja kabla ya kutoa taarifa ya kuyahamishia Pemba.

Uwanja huo ni miongoni mwa viwanja vinavyotarajiwa kutumiwa kwa ajili ya mashindano ya Chan

Katika taarifa iliyotolewa jana Aprili 21, 2025 na Kaimu Ofisa Habari wa ZFF, Issa Chiwilem, imesema kuwa ZFF imepokea barua pepe (email) kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) juu ya maelekezo ya kitaalamu ya matumizi ya uwanja huo.

"Uwanja wa New Amaan Complex kwa sasa umeingia katika mfumo maalumu wa matumizi, taarifa ya CAF imebainisha kuwa uwanja huo haushauriwi kuchezwa kwa mashindano yenye mechi nyingi mfululizo," imesema taarifa hiyo.

Hivyo katika kutekeleza agizo hilo, taarifa hiyo imesema mashindano ya Muungano mwaka huu yatachezwa Gombani kisiwani Pemba

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamethibitisha kushiriki michuano hiyo mwaka huu ambapo April 26 watacheza mechi ya robo fainali dhidi ya KVZΒ 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’