Mzize, Dube wapigiwa chapuo ufungaji bora

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Apr 2025
Mzize, Dube wapigiwa chapuo ufungaji bora

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi anatamani kuona tuzo ya mfungaji bora ligi kuu ya NBC msimu huu inachukuliwa na mchezaji wa Yanga

Mpaka sasa mshambuliaji Clement Mzize ndiye anayeongoza mbio hizo akiwa amefunga mabao 13 lakini anachuana vikali na mshambuliaji mwenzake Prince dube aliyefunga mabao 12 kama ilivyo kwa Jean Ahoua wa Simba ambaye pia amefunga mabao 12

Katika orodha hiyo pia yupo mshambuliaji wa Singida Black Stars Jonathan Sowah aliyepachika mabao 11. Sowan amecheza mechi 10 tu akitua Singida Black Stars katika dirisha dogo la usajili

Pacome Zouzoua wa Yanga nae yumo akifunga mabao 9 huku mfungaji bora wa msimu uliopita Aziz Ki akifunga mabao 8

Hamd amesema Mzize na Dube wana nafasi ya kushinda tuzo hiyo na kwake angependa kuona tuzo hiyo inarejea tena Jangwani

"Nimewaambia washambuliaji wangu kama sio Dube, basi Mzize lazima wahakikishe wanachukua Tuzo ya Mfungaji Bora na ili waweze kulifanikisha hilo wanatakiwa kuendelea kutumia nafasi"

"Hata wachezaji wenzao sasa wanawarahisishia kazi uwanjani kwa kuwatengenezea nafasi za kufunga zaidi, lakini pia mfumo wa timu namna inavyocheza haitakuwa na kisingizio kwao kutokuwa juu kwa ufungaji," alisema Hamdi

Kwa misimu miwili mfululizo , Yanga imetoa mfungaji bora na mchezaji bora wa msimu, baada ya Fiston Mayele kubeba tuzo hizo, Aziz Ki akabeba msimu uliopita

Aidha Ki alimtabiria Dube kuwa anaweza kushinda tuzo hiyo. Yanga ina mechi tatu za kuhakikisha tuzo hiyo inabaki Jangwani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’