Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es Salaam leo Ijumaa kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya ushiriki wa michuano ya Kombe la Muungano 2025 iliyoanza jana
Yanga imepangwa kuvaana na KVZ kesho Jumamosi katika mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo iliyorejeshwa msimu uliopita
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa hawaendi kushiriki tu michuano hiyo, bali dhamira yao ni kurejea na kombe Dar es salaam
"Tunawaambia tu, wenyeZanzibar yetu tinakuja, msimu huu tumesema hatuachi kitu," alitamba Kamwe
Michuano hiyo inafanyika kisiwani Pemba katika uwanja wa Gombani
ADVERTISE HERE