Baada ya kuitumikia Yanga kwa takribani misimu miwili na nusu, hatma ya mshambuliaji Kennedy Musonda iko mikononi mwa kocha Miloud Hamdi
Ifikapo mwezi Juni 2025, Musonda atakuwa mchezaji huru kwani mkataba wake na Yanga utakuwa umemalizika
Wakati mkataba wake ukielekea ukingoni, hakuna mazungumzo yaliyofanyika kuhuisha mkataba huo
Yanga inahusishwa kumuwania mshambuliaji wa Singida Black Stars Jonathan Sowah, ni wazi Mghana huyo huenda akachukua nafasi yake
Msimu wake wa kwanza na Yanga chini ya kocha Nasreddine Nabi ulikuwa na mafanikio zaidi pengine kuliko nyakati za makocha waliofuata Miguel Gamondi, Sead Ramovic na sasa Hamdi
Msimu huu amekuwa na muda mchache zaidi uwanjani kutokana na majeraha ya mara kwa mara huku Prince Dube na Clement Mzize wakionekana kufanya vizuri zaidi yake