Kikosi cha Yanga kilitua Pemba mapema jana na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa Wananchi waliokuwa wakiisubiri kwa hamu timu yao
Leo saa 1:15 usiku Yanga itakuwa dimbani Gombani kuikabili KVZ katika mchezo wa robo fainali
Wananchi wanaitaka nusu fainali, ambapo kama watashinda leo, katika hatua hiyo watakutana na JKU iliyoiondosha Coastal Union jana
Vijana wa kocha Miloud Hamdi walikamilisha maandalizi yao katika uwanja wa Gombani jana usiku, tayari kwa mchezo huo








ADVERTISE HERE