Kesho Jumanne, April 29 kikosi cha Yanga kitashuka tena uwanja wa Gombani, Pemba kuikabili Zimamoto katika mchezo wa nusu fainali ya ligi ya Muungano
Ushindi katika mchezo huo utawahakikishia Wananchi kutinga fainali na kuwa katika nafasi ya kushinda taji la pili msimu huu
Yanga tayari ina Ngao ya Jamii na pengine msimu huu inaweza kubeba mataji manne
Wananchi wako kileleni mwa msimamo wa ligi kuu wakisalia na mechi tatu za kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo
Kikosi cha kocha Miloud Hamdi pia kiko hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho la CRDB ikitarajiwa kucheza dhidi ya JKT Tanzania mchezo utakaopigwa kati ya May 16-18 dimba la Mkwakwani Tanga kuwania tiketi ya fainali
Msimu huu unaweza kuwa wa kipekee kwa Wananchi kama watafanikiwa kutimiza malengo kwa asilimia 100
Ipo kauli isemayo kinachotofautisha timu kubwa na ndogo ni idadi ya makombe ambayo yako kabatini