Katika msimu huu wa ligi kuu ya NBC, Yanga imefunga jumla ya mabao 68 huku ikiruhusu mabao 10 katika mechi 26
Katika mabao hayo ya kufunga, 55 yamefungwa ndani ya 18 huku mengine 13 yakifungwa nje ya eneo la hatari
Takwimu zinaonyesha Yanga ndio timu iliyofunga mabao mengi zaidi kutokea ndani ya 18
Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani mabingwa hao wa nchi ni hatari wanapoingia ndani ya 18 wakifunga idadi kubwa mabao katika eneo hilo
Yanga ndio vinara wa ligi kuu ya NBC wakikusanya alama 70, alama 13 juu ya watani zao Simba wanaoshika nafasi ya pili
Yanga iinahitaji kushinda mechi tatu zilizosalia ili kujihakikishia ubingwa wa nne mfululizo ambao utakuwa ubingwa wa 31
Kuhusu mchezo dhidi ya Simba, kesi bado inaunguruma CAS huku uongozi wa Yanga ukiweka msimamo wa kutocheza mechi hiyo namba 184 ambayo iliahirishwa kinyume na kanuni
