Nahoda msaidizi wa Yanga Dickson Job ni miongoni mwa wachezaji ambao wanamaliza mikataba mwishoni mwa msimu lakini habari njema ni kuwa Yanga imepiga hatua nzuri katika mazungumzo ya kumuongeza mkataba
Licha ya kupokea ofa kutoka klabu za ndani na nje ya nchi, Job ameipa kipaumbele Yanga na makubaliano ni kuwa atasaini mkataba kuendelea kuitumikia Yanga
Aidha kiungo Mudathir Yahya naye mkataba wake uko ukiongoni, licha ya ofa nono kutoka Azam Fc, Mudathir amewahakikishia mabosi wa Yanga ataendelea kusalia Jangwani
Viungo washambuliaji Maxi Nzengeli na Pacome Zouzoua walishakamilisha mazungumzo ya mikataba mipya, kilichokuwa kikisubiriwa ni kukamilika taratibu za kusaini mikataba yao
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewatoa hofu wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa wachezaji wote wanaohitajika kuendelea kuitumikia Yanga wataongezwa mikataba
Nyota wengine ambao mikataba yao inaelekea ukingoni na pamoja na Khalid Aucho, Kennedy Musonda, Yao Kouassi na Clatous Chama
Aucho huenda akaongeza mwaka mmoja huku hatma ya Musonda na Chama akisalia mikononi mwa kocha Miloud Hamdi ambaye atawasilisha ripoti yake baada ya msimu kumalizika