Baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Muungano visiwani Zanzibar, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu unaofuata dhidi ya Namungo Fc
Jumanne ya May 13, Yanga itakuwa mwenyeji wa Namungo Fc katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa KMC Complex
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema mkakati uliopo ni kuhakikisha wanashinda mechi zote zilizobaki ili kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo
"Shamra-shamra za ubingwa wa Muungano zimemalizika sasa tunarejea katika maandalizi ya mechi za kuhitimisha msimu"
"Tuna mechi tatu za ligi kuu lakini pia tuna mechi ya nusu fainali ya kombe la CRDB dhidi ya JKT Tanzania"
"Melengo yetu ni kuona tunatetea mataji yote mawili ambayo tunayashikilia kwa misimu mitatu," alisema Kamwe
Mechi tatu za ligi kuu zilizobaki ni dhidi ya Namungo Fc (May 13), Tanzania Prisons (May 21) na Dodoma Jiji (May 25) hata hivyo kuna uwezekano mkubwa yatafanyika mabadiliko ya ratiba kwa mechi mbili za mwisho
Mchezo wa nusu fainali kombe la CRDB utapigwa kati ya May 15-18 mkoani Tanga katika uwanja wa Mkwakwani