Afya ya kiungo fundi wa Yanga Khalid Aucho imeimarika na huenda akauwahi mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumanne ijayo, May 13 katika uwanja wa KMc Complex
Aucho amekosekana katika kikosi cha Yanga kwa takribani wiki tatu akisumbuliwa na nyama za paja, majeraha ambayo alipata kwa mara ya kwanza wakati akiitumikia timu ya Taifa
Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Uganda amepata muda wa kutosha 'ku-recover', sasa ameimarika na tayari kwa mechi za kuhitimisha msimu
Kwa kuzingatia msimamo wa Yanga, mechi zilizobaki kwenye ligi ni tatu dhidi ya Namungo Fc, (May 13), Tanzania Prisons(Juni 18) na Dodoma Jiji (Juni 22) pamoja na mchezo wa nusu fainali kombe la CRDB dhidi ya JKT Tanzania (May 18)
Kuhusu mchezo dhidi ya Simba, uongozi wa Yanga umeweka msimamo kuwa wataendelea kuipambania haki yao kwa njia nyingine baada ya kukosa imani na wenye mamlaka ya uendeshaji wa soka nchini katika kutatua mgogoro wa mechi namba 184