Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema nyota wote waliokuwa na changamoto za majeruhi wamerejea mazoezini tayari kwa mechi za kuhitimisha msimu
Kikosi cha Yanga jana kiliendelea na mazoezi KMC Complex kujiandaa na mchezo unaofuata wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa Jumanne, May 13
"Tunashukuru wachezaji waliokuwa na changamoto za majeruhi wamerejea kuendelea na majukumu yao"
"Khalid Aucho alikuwa na shida ya nyama za paja lakini kama mnavyomuona sasa yuko sawa kama ilivyo kwa Pacome Zouzoua na Kennedy Musonda ambaye alipata changamoto katika michuano ya ligi ya Muungano"
"Mchezaji pekee ambaye bado anaendelea na program maalum ni Yao Kouassi, taarifa kuhusu ni wakati gani atakuwa tayari kutumika tutaitoa baadae," alisema Etutu
Katika mwezi May, Yanga itacheza mechi mbili kwani baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc May 13, mchezo utakaofuata ni nusu fainali kombe la CRDB dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa uwanja wa Mkwakwani, May 18