Mapema leo Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said akiwa sambamba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa Bunge jijini Dodoma kushuhudia uwasilishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2025 / 2026
Wakati Injinia Hersi anatambulishwa, ziliibuka shangwe kutoka kwa Wabunge huku baadhi yao wakisikika wakisema 'HATUCHEZI'
Yanga imetangaza msimamo wa kutocheza mchezo wa ligi kuu namba 184 dhidi ya Simba ambao umepangwa kupigwa Juni 15

ADVERTISE HERE