Kiwango bora alichokionyesha kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua katika mwezi April 2025, kimempa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi tuzo inayodhaminiwa na NIC
Kabla ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Azam Fc, Pacome aliweka rekodi ya kushinda tuzo tatu mfululizo za mchezaji bora wa mechi pia akifunga na kutoa pasi za mabao
Pacome amekuwa na msimu bora akifunga mabao 9 na kutoa pasi nane za mabao katika ligi kuu ya NBC
Kwa kushinda tuzo hiyo Pacome pia ataondoka na kitita cha Tsh Milioni 4 kutoka kwa Wadhamini NIC

ADVERTISE HERE