Baada ya kukosekana katika michuano ya ligi ya Muungano, mshambuliaji wa Yanga Prince Dube amerejea kikosini akiwa sehemu ya kikosi kinachoendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa Jumanne, May 13 katika uwanja wa KMC Complex
Dube, Duke Abuya na Clatous Chama walikosa michuano hiyo wakipewa ruhusa kushughulikia masuala ya kifamilia huku Khalid Aucho, Pacome Zouzua na Yao Kouassi nao wakikosekana wakiwa majeruhi
Wote wamerejea isipokuwa Yao ambaye bado anaendelea na program maalum ya mazoezi huku timu ya madaktari ikijiridhisha na utayari wake kabla ya kumruhusu kujumuika na wenzake
Katika mechi tatu zilizobaki, Dube ana kazi ya kupambana kuisaka tuzo ya ufungaji bora akiwa nyuma kwa mabao matatu dhidi ya Jean Ahoua wa Simba anayeongoza na mabao 15 huku Clement Mzize akifuatia na mabao 13
Dube hakuanza vyema msimu huu lakini kufunga mabao 12 na kutoa pasi 8 za mabao ni mafanikio makubwa kwake
Katika moja ya mahojiano yake, Dube alisema jambo muhimu kwake ni kuhakikisha anaisaidia Yanga kushinda mechi na kufikia malengo yake
Kuhusu ufungaji bora sio jambo alilopanga lakini lolote linaweza kutokea katika mechi zilizobaki