Yanga inaweka rekodi ya kibabe kombe la FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 May 2025
Yanga inaweka rekodi ya kibabe kombe la FA

Klabu ya Yanga SC inaendelea kuandika historia katika soka la Tanzania, huku ikielekea katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CRDB Cup) kwa msimu wa 2024/2025

Tarehe 18 Mei 2025, Wananchi watashuka dimbani kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, kumenyana na JKT Tanzania katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kuvutia.

Yanga, mabingwa watetezi wa michuano hii kwa misimu mitatu mfululizo, wanawania kuweka rekodi ya kipekee ya kutwaa taji hili kwa msimu wa nne mfululizo

 Hii siyo tu safari ya kutetea ubingwa, bali pia ya kutafuta fainali ya tano mfululizo, jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye historia ya CRDB Cup.

Tangu wapoteze fainali dhidi ya Simba SC kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Lake Tanganyika mnamo Julai 25 2021, Yanga hawajapoteza mchezo wowote wa michuano hii. Kwa sasa, wameweka rekodi ya ushindi wa mechi 23 mfululizo kwenye CRDB Cup, wakionyesha ubabe na uimara wa kikosi chao katika kila hatua

Kwa upande mwingine, JKT Tanzania wanakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuzuia kasi hii ya Yanga. Wananchi hawajaficha dhamira yao – kutinga fainali nyingine na ikiwezekana, kukutana na watani zao wa jadi, Simba SC, katika fainali nyingine ya michuano hiyo

Historia ya Mafanikio ya Yanga SC kwenye CRDB Cup

Hapa chini ni muhtasari wa mafanikio ya Yanga tangu waanze kutawala michuano hiyo:

  • Msimu wa 2021/2022
    Yanga waliibuka mabingwa kwa ushindi mnono dhidi ya Coastal Union kwenye fainali. Ushindi wa mikwaju ya penati 4-1 baada ya sare ya mabao 3-3

  • Msimu wa 2022/2023
    Wananchi walirudia ubingwa wao kwa kuifunga Azam FC bao 1-0 katika fainali iliyochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

  • Msimu wa 2023/2024
    Fainali ya kusisimua dhidi ya Azam FC dimba la New Amaan Complx, iliwaweka tena Yanga kwenye orodha ya mabingwa. Mechi hiyo ilihitimishwa kwa mikwaju ya penalti 6-5 baada ya suluhu ya bila kufungana ndani ya dakika 120.

  • Msimu wa 2024/2025 (inaendelea)
    Yanga wapo hatua ya nusu fainali wakisaka rekodi ya kutwaa kombe hili kwa mara ya nne mfululizo na pia fainali ya tano mfululizo. Wameonyesha kiwango bora na kuendeleza rekodi ya kushinda mechi 23 mfululizo kwenye michuano hii tangu Julai 2021

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’