Julai 27 visiwani Zanzibar kuna mechi ya kibabe kati ya wakongwe waliowahi kutamba timu ya Taifa Zanzibar dhidi ya wenzao waliowahi kutamba na timu ya Taifa ya Brazil
Ndio! mechi hii iliyopewa jina la 'Match of the Legends' itamleta Zanzibar fundi wa mpira Ronaldinho Gaucho na malegendari wenzake wa Brazil kama Rivaldo, Kaka, Cafu, Roberto Carlos, Ronaldo De Lima na wengine kibao
Yanga kama mdau rasmi wa kutangaza utalii wa Zanzibar, itahusika katika kuitangaza mechi hiyo 'promotion' ambapo Meneja wa Habari na Mawasiliano Ali Kamwe na kitengo chake wamepewa jukumu la kuutangaza mchezo huo
Kamwe amedokeza kuwa Yanga imekamilisha usajili wa kiungo mmoja mahiri hapa nchini na amemuomba Rais wa Yanga Injinia Hersi Said awaruhusu wamtumie nahodha wa kikosi cha wakongwe wa Brazil Ronaldiho kumtambulisha kiungo huyo
"Yanga kama mdau rasmi wa kutangaza utalii Zanzibar jukumu letu ni pamoja na kuitangaza mechi hii"
"Katika moja ya matukio tuliyoandaa, kama itampendeza Rais Injinia Hersi Said tumtumie Ronaldinho kumtambulisha yule kiungo tuliyemsajili kwa kuwa mechi hii itapigwa dirisha la usajili likiwa limefunguliwa"
"Tunaona itakuwa vyema kama mkongwe fundi wa mpira Ronaldinho Gaucho atamtambulisha fundi anayetua kucheza katika eneo kama lake," alisema Kamwe
Tetesi zinamhusisha kiungo wa Azam Fc Feisal Salum 'Fei Toto' kuwa mbioni kurejea kwa waajiri wake hao wa zamani