Mara paap! Mokwena huyu hapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 May 2025
Mara paap! Mokwena huyu hapa

Klabu ya Yanga SC inaonekana kuingia kwenye sura mpya ya mipango yake ya ushindani katika ngazi ya juu ya soka la Afrika baada ya kuhusishwa moja kwa moja na mazungumzo na kocha mahiri kutoka Afrika Kusini, Rulani Mokwena.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo zimethibitisha kuwa Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amefanya mazungumzo ya awali na Mokwena, ambaye hivi karibuni aliachana na Wydad Athletic Club ya Morocco.

MILOUD HAMDI KWENYE MKONDO WA KUONDOKA

Mkataba wa kocha wa sasa wa Yanga, Miloud Hamdi, unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu huku kukiwa na dalili kwamba anaweza kuondoka

Hamdi aliajiriwa kama suluhisho la muda mfupi kufuatia kuondoka kwa Sead Ramovic, amekuwa na kipindi cha mafanikio lakini ni wazi hatma yake itategemea mazungumzo mapya baada ya mkataba wake kufika mwisho.

Vyanzo vya ndani vinasema kuna uwezekano mkubwa Hamdi akarejea katika klabu ya Singida Black Stars kuendeleza mradi aliokuwa ameuanzisha kabla ya 'kunyakuliwa' na Yanga

MOKWENA: KOCHA WA KISASA NA MAONO MAKUBWA

Kwa upande mwingine, jina la Rulani Mokwena limekuwa kivutio kwa wadau wengi wa soka kutokana na mafanikio yake akiwa na Mamelodi Sundowns, ambako alijijengea sifa ya kuwa na falsafa ya soka ya kisasa, inayotawaliwa na nidhamu, mbinu sahihi na maendeleo ya wachezaji chipukizi.

Ingawa muda wake na Wydad ulikuwa mfupi, ameisaidia klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye ligi ya Morocco na kufuzu CAF Confederation Cup (CAF CC) – hatua ambayo inachukuliwa kama mafanikio ukizingatia hali ya awali ya klabu hiyo kabla ya kuwasili kwake.

MALENGO YA YANGA: UBINGWA WA AFRIKA

Kwa muda mrefu, Yanga imekuwa na ndoto ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika – ndoto ambayo imekuwa ikipata misukosuko kutokana na ukosefu wa uthabiti kwenye benchi la ufundi.

Kuja kwa kocha kama Mokwena ambaye ana rekodi inyovutia hasa wakati yuko Mamelodi, kunaweza kuwa hatua madhubuti ya kuimarisha kikosi kuelekea mafanikio hayo

Wakati mwingine makocha hawaangalii maslahi pekee, bali pia miundombinu na mfumo wa kiutendaji ndani ya klabu. Yanga ni miongoni mwa klabu chache zinazoendeshwa kisasa barani Afrika. Sasa ina uwezo wa kusajili wachezaji bora na mazingira yake yanaweza kumshawishi kocha yeyote kujiunga nayo

Mokwena anaweza kuwa alama mpya ya mabadiliko makubwa, hasa katika kuhakikisha timu inavuka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na kupata mafanikio makubwa zaidi kuliko miaka ya nyuma.

Ikiwa mazungumzo haya yatazaa matunda, basi Yanga SC itakuwa imepiga hatua kubwa katika safari yake ya kuwa miongoni mwa vigogo wa soka la Afrika.

Rulani Mokwena si kocha wa kawaida – ni mbunifu, kijana mwenye njaa ya mafanikio, na anayeelewa vema ramani ya soka la kisasa.

Endapo dili hili litakamilika, itakuwa ni hatua kubwa na yenye uzito mkubwa si kwa Yanga pekee, bali kwa soka la Tanzania kwa ujumla

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’