Kocha Msidizi wa Yanga U20 Ali Kamwe amekiri kuwa wamepoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya ligii ya vijana U20 hapo jana baada ya kuzidiwa kimbinu wa wapinzani wao
Licha ya kucheza pungufu kwa zaidi ya dakika 60, vijana wa Tanzania Prisons waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga U20 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Akizungumza baada ya mchezo huo, Kamwe alikiri Prisons walikuwa bora zaidi kuliko wao na wanatambua wana kazi ya kufanya ili kuhakikisha wanashinda mechi mbili zilizobaki
"Nikiri wapinzani wetu walikuwa bora licha ya kucheza muda mrefu wakiwa pungufu. Sisi tulikosa umakini hasa tuliposhambulia wachezaji wetu walipanda mbele pasipo kuchukua tahadhari"
"Matokeo yake tuliacha mianya ambayo wapinzani wetu waliitumia kupitia mashambulizi ya kushitukiza kutuadhibu"
"Tunakwenda kufanyia kazi mapungufu tuliyoyaona ili kuhakikisha tunashinda mechi mbili zilizosalia ili tuwe naa nafasi ya kusonga mbele hatua ya robo fainali," alisema Kamwe
Kesho Alhamisi Yanga itacheza mechi ya pili dhidi ya Fountain Gate na kisha kumaliza mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Kagera Sugar May 24