Beki wa kati wa Yanga Princess Uzoamaka Confidence Igwe ameibuka kuwa mchezaji bora wa msimu wa Yanga Princess 2024/25
Usiku wa jana Yanga iliandaa hafla ya kuwatuza wachezaji wa Yanga Princess waliofanya vyema msimu huu wa ligi ya Wanawake ambao ulifikia tamati juzi kwa Yanga Princess kumaliza katika nafasi ya tatu
Uzoamaka raia wa Nigeria amekuwa na msimu bora katika kikosi cha Yanga Princess akiongoza safu ya ulinzi
Tuzo maalum ya heshima ilikwenda kwa Aisha Masaka, mshambuliaji wa zamani wa Yanga Princess ambaye kwa sasa anachezea kunako klabu ya Brighton ambayo inashiriki ligi kuu soka Nchini Uingereza

Jeanine Mukandayisenga akatwaa tuzo ya ufungaji bora. Jeanine aliyetua Yanga Princess kwenye usajili wa dirisha, alipachika mabao 13 mabao 10 akiyafunga katika WPL
Angela Michael yeye akashinda tuzo maalum huku tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu ikienda kwa Rrita Akarreko



Kalsa Aregash yeye aliondoka na tuzo ya goli bora la msimu