Ndivyo unavyoweza kusema baada ya timu ya vijana ya Yanga kuaga mapema michuano ya ligi ya vijana baada ya kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Fountain Gate Youth katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex jana
Hicho kilikuwa kipigo cha pili kwa Yanga U20 ambayo ilikubali kipigo cha mabao 2-1 katika mechi ya kwanza na sasa inaburuza mkia kundi B
Yanga U20 inayonolewa na Kocha Vicent Barnabas huku Ali Kamwe akiwa sehemu ya benchi la ufundi hilo kama kocha msaidizi, watakamilisha mechi ya mwisho dhidi ya vinara Kagera Sugar lakini hata wakishinda hakuna nafasi ya kusonga mbele hatua ya robo fainali
Kagera Sugar inaongoza kundi B ikiwa na alama 4 sawa Fountan Gate huku Prisons ikishika nafasi ya tatu na alama 3
Akizungumza baada ya kupoteza mechi ya pili mfululizo, Kamwe alisema walikosa bahati tu katika mechi zote mbili walizopoteza kwani vijana walipambana lakini pia waliadhibiwa kutokana na makosa madogo madogo ya kiufundi