Mkurugenzi wa Wanachama na Masoko wa Yanga SC, Ibrahim Samuel amewataka wanachama na mashabiki kulipa ada zao kwa wakati kwani wao ndio chachu ya maendeleo ya klabu
Samuel amewataka wale ambao bado hawajasajiliwa kama wanachama au mashabiki wajiunge katika matawi kujisajili na kutambulika rasmi na klabu
Akizungumza katika semina ya viongozi wa matawi iliofanyika Kigamboni jana, Samuel alisema mpaka sasa jijini Dar es salaam kuna matawi 271 ambayo yamekidhi vigezo na kutambulika na klabu
Amesema Matawi yana nguvu kubwa kwenye ukuaji wa klabu kwani huko ndipo ambapo maoni ya namna gani ya kuendesha klabu yanaweza kutolewa
"Tumetengeneza michakato mbalimbali bora kabisa ili kuhamasisha ulipaji wa ada kwa Mkoa wa Dar es Salaam .Tulianza na matawi 91. Idara ya wanachama tukaja na ubunifu ambao ulizalisha matawi mapya.Tulikwenda vyuoni tukaanzisha Young Z na tulitembelea taasisi mbalimbali. Hivi sasa tuna matawi 271 yaliyo hai"
"Matawi yana nguvu kubwa sana kwenye ukuaji wa klabu yetu. Huku ndipo ambapo maoni ya namna gani ya kuendesha klabu yetu yaanzia. Ndio maana kwenye matawi huwa tunawasisitiza sana muwe mnafanya vikao vya mara kwa mara. Viongozi wa matawi pia wana wajibu mkubwa kuhakikisha kuwa wanasoma katiba ya klabu ili kutambua majukumu yao," alisema
Katika semina hiyo pia kulikuwa na zoezi la uandikishaji Wanachama na Mashabiki ambapo Samuel alikabidhi kadi kwa wanachama na mashabiki wapya