Yanga imeshindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa saba mfululizo baada ya kuchapwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye dimba la Jamhuri mkoani Morogoro.
Bao pekee la Mtibwa Sugar lilifungwa na kiungo wa zamani wa Yanga Hassani Dilunga kwa shuti kali la chinichini akiwa ndani ya 18.
Tofauti na mchezo dhidi ya Prisons, kikosi cha Yanga leo kilikuwa kimeimarika zaidi na kuweza kuhimili mikikimikiki ya Mtibwa Sugar.
Yanga ilipoteza nafasi mbili muhimu kupitia mashuti ya Thabani Kamusoko na Matheo Antony ambayo yote iligonga miamba.
Hicho ni kipigo cha tatu mfululizo kwa kikosi cha Yanga kwenye ligi kuu ya Vodacom.
Yanga inarejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Rayon Sport.
Sehemu kubwa ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Yanga walibaki jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa Jumatano ijayo kwenye uwanja wa Taifa

ADVERTISE HERE