Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema klabu ilishawasilisha msimamo wake kwa Bodi ya Ligi wa kutocheza mechi namba 184 ya ligi kuu dhidi ya Simba iliyopangwa kucheza Juni 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kauli hiyo ya Kamwe imekuja siku moja baada ya Msemaji wa Bodi ya Ligi Karim Boimanda kunukuliwa na vyombo vya habari akidai hawajapokea taarifa yoyote kutoka kwa klabu ya Yanga kuhusu kutocheza mchezo huo
Kamwe amesema wamekuwa na Mawasiliano na TPLB, wamewasilisha madai yao ambayo wanahitaji majibu kutoka kwa Bodi
"Msimamo wetu kama klabu kuhusu mchezo namba 184 uko wazi, yote ambayo yanahitajika yameshawasilishwa kwa Bodi ya Ligi na tunasubiri kuona majibu"
"Kwa sasa hatuwezi kuzungumza hadharani ni kitu gani ambacho Yanga imehitaji, lakini ifahamike Yanga tayari imeshatoa msimamo wake na tayari kumeshakuwa na njia za kuzungumza na kuwasilisha hilo"
"Sasa kama wao wanasema hawajapokea taarifa yoyote kutoka kwetu basi kuna changamoto, sisi tunazungumzia upande wetu, tunafanya mawasiliano na Bodi ya ligi na taarifa zetu zinakwenda huko," alisema Kamwe