Wazee wametoa maagizo haya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jun 2025
Wazee wametoa maagizo haya

Pamoja na kusisitiza kuwa Juni 15 Yanga haitakwenda uwanjani kucheza mechi namba 184 dhidi ya Simba, Wazee wa Yanga pamoja na viongozi wa Matawi wametangaza msimamo kuwa hakuna Mwanayanga yeyote ambaye anapaswa kwenda uwanjani Juni 15

Hii ni pamoja na viongozi wa klabu, yeyote ambaye atajaribu kuipeleka timu uwanjani basi afahamu atakuwa amejiondoa mwenyewe katika uongozi

Pia Wazee wamepiga marufuku Yanga kutajwa na chombo chochote cha habari kinachofanya matangazo ya mchezo huo

Kuhusu suala la Simba kupewa alama tatu na Yanga kupokwa alama 15, Wazee wamebainisha kuwa hawatarajii Yanga kupokwa alama na Bodi ya ligi kwa kuwa kama watafanya hivyo watathibitisha malalamiko ya Yanga kutokuwa na imani na Bodi hiyo ikizingatiwa hawakuchukua hatua kama hiyo March 08 pale Simba ilipoingia mitini

Mpaka sasa Bodi ya ligi haijajibu madai ya Yanga kwa kuzingatia barua ya klabu iliyoandikwa kwa Bodi hiyo March 09. Miongoni mwa madai ya Yanga ni kupewa alama tatu za mchezo huo kwa mujibu wa kanuni

Zaidi Wazee wamesema kama Bodi itachukua hatua ya kuipoka Yanga pointi, basi huo ndio utakuwa mwisho wa msimu huu

"Tarehe 15 ndio itatoa taswira ya mechi yetu ya juni 18, tukipokonywa hizo alama 15 ligi itakuwa imeishia hapo kwanza hakuna Kiongozi wa kutupokonya sisi alama 15 yaani wakijaribu tu ligi itakuwa imeisha," Shabani Omary Mgonja Mzee wa Yanga ambaye pia ni Mratibu wa Matawi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’