Yanga kuifuata Prisons mapema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jun 2025
Yanga kuifuata Prisons mapema

Klabu ya Yanga SC imefanya mabadiliko kwenye ratiba yake huku ikielekeza nguvu zake zote katika mechi tatu za mwisho za kumaliza msimu wa 2024/25. Mabosi wa klabu hiyo wamefuta safari ya kuelekea Rwanda ambako walikuwa wamepanga kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports Juni 15.

Kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe, mpango huo sasa umepelekwa mbele hadi wakati wa maandalizi ya msimu ujao wa 2025/26 (pre-season), ambapo Yanga itapanga ratiba mpya ya maandalizi na michezo ya kirafiki.

Katika kipindi hiki, Yanga imeamua kuelekeza nguvu na akili kwenye mechi tatu muhimu zinazoikamilisha rasmi kampeni yao ya msimu huu. Mechi mbili ni za ligi kuu dhidi ya Prisons n Dodoma Jiji wakati mchezo mmoja ni fainali ya kombe la CRDB dhidi ya Singida BS

Kamwe amethibitisha kuwa kikosi cha Yanga kitaondoka jijini Dar es Salaam mnamo Juni 15 kuelekea Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mechi dhidi ya Tanzania Prisons itakayopigwa Juni 18. Timu hiyo itakuwa na siku mbili za kujiandaa na mchezo huo ukiwa ni sehemu ya ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga imesisitiza msimamo wa kutocheza mechi namba 184 ya Ligi Kuu dhidi ya Simba SC, ambayo ilipangwa kupigwa Juni 15, hadi hapo Bodi ya Ligi itakapotoa uamuzi kuhusu madai ya klabu hiyo kuhusiana na mechi hiyo ambayo awali ilipaswa kuchezwa Machi 8.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
30m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
48m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
54m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’