Klabu ya Yanga SC inaendelea na maandalizi ya mechi zake tatu za mwisho wa msimu, mbili za Ligi Kuu Bara na moja ya Kombe la Shirikisho
Mabingwa hao watetezi NBC PL wameanza mikakati ya mapema ya kuimarisha kikosi kwa msimu ujao
Katika harakati hizo, Yanga inatajwa kuiwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Tabora United, Offen Chikola kuongeza mafundi wazawa.
Chikola, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na Yanga, anamaliza mkataba na Tabora United mwishoni mwa msimu
Usajili wa Chikola ni sehemu ya mkakati wa kuongeza ushindani katika safu ya kiungo cha ushambuliaji
Chikola atakabiliwa na ushindani kutoka kwa wachezaji kama Maxi Nzengeli, Clement Mzize na Farid Mussa ambaye hata hivyo anaweza kutolewa kwa mkopo, huku Singida Black Stars na Mbeya City zikitajwa kumuhitaji
Kwenye msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC, Chikola amefunga mabao saba. Hii inaweka ushindani mkali ndani ya Yanga, kwani Maxi Nzengeli ana mabao matano na asisti tisa, huku Mzize akiwa na mabao 13 na asisti tatu.