Nyota Yanga waliokuwa Stars kurejea leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Jun 2025
Nyota Yanga waliokuwa Stars kurejea leo

Wachezaji watatu wa Yanga waliokuwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wameruhusiwa kurejea nchini kuungana na wenzao katika maandalizi ya mechi za kuhitimisha msimu

Jana Stars ilipimana ubavu na Afrika Kusini katika mchezo uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana. Dickson Job na Ibrahim Bacca walikuwa sehemu ya kikosi kilichoshuka dimbani huku Shekhan Khamis akiwa sehemu ya wachezaji wa akiba

Taarifa imeeleza kuwa wachezaji hao wameruhusiwa kuwahi maandalizi ya mchezo namba 184 wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopangwa kupigwa Juni 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Hata hivyo msimamo wa Yanga uko wazi, hawatacheza mchezo huo kama Bodi ya ligi haitajibu malalamiko waliyowasilisha kwa Bodi hiyo March 09

Bodi hiyo pia imetakiwa kuweka hadharani majibu ya uchunguzi waliofanya ili kubainisha sababu zilizopelekea wahirishe mchezo huo uliopaswa kupigwa March 08

Kwa sasa kikosi cha Yanga kinajiandaa na mechi mbili za kumaliza msimu dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji pamoja na mchezo wa fainali kombe la CRDB dhidi ya Singida BS utakaopigwa Juni 28 visiwani Zanzibar

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’