Hatutaki kuacha kombe lolote - Aucho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jun 2025
Hatutaki kuacha kombe lolote - Aucho

Kiungo mahiri wa Klabu ya Yanga, Khalid Aucho, ameweka bayana dhamira ya timu hiyo maarufu kutoka Jangwani ni kutetea makombe yote mawili yaliyobaki yaani Ligi Kuu ya NBC na Kombe la CRDB (FA).

Kwa msisitizo mkubwa, Aucho amesema kuwa lengo kuu ni kushinda kila mechi iliyosalia, bila kuacha nafasi yoyote ya kupoteza pointi.

Yanga SC, ambayo imepania kutwaa taji la Ligi Kuu kwa mara ya nne mfululizo, inakabiliwa na mechi mbili ngumu dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji. Aidha, mbele yao pia kuna fainali ya Kombe la CRDB dhidi ya Singida Black Stars, itakayochezwa visiwani Zanzibar Juni 28.

"Mechi zilizobaki ni muhimu sana kwetu ili kutimiza malengo yetu. Tutahakikisha tunashinda zote," alisema Aucho kwa msisitizo.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uganda aliongeza kuwa, pamoja na hali ya sintofahamu kuhusu mchezo dhidi ya Simba SC unaopangwa Juni 15, wao kama Yanga wako tayari kwa lolote.

"Siwezi kuzungumzia kuhusu mechi dhidi ya Simba kutokana na hali ilivyo, lakini nikuhakikishie tuko tayari hata kama itaamuliwa ichezwe. Hatuwahofii," alisema kwa kujiamini.

Kikosi cha Yanga tayari kimerejea kambini, kikitoka katika mapumziko ya takribani siku 10. Maandalizi yameshika kasi chini ya Kocha Mkuu Miloud Hamdi, ambaye amesisitiza kuwa mkakati ni kutetea mataji hayo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’