Kiungo wa Yanga Jonas Mkude huenda akajiunga na klabu ya KMC pale mkataba wake na Wananchi utakapomalizika, imefahamika
Mkude atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa mwezi huu kwani kandarasi yake na Yanga itafikia tamati huku kukiwa hakuna mazungumzo ya kuhuisha mkataba wake
Kiungo huyo mkongwe ameitumikia Yanga kwa misimu miwili akitokea klabu ya Simba
Hata hivyo msimu huu amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza jambo linaloashiria hakuna uwezekano wa kuongeza mkataba
Yanga inatarajiwa kufanya maboresho ya kikosi chake ambapo baadhi ya wachezaji waandalizi wanaomaliza mikataba huenda wakapewa mkono wa kwaheri
ADVERTISE HERE